Kamati Kuu ya chama tawala nchini Tanzania,(CCM) inakutana leo Jumamosi jijini Dar es salaam, katika ajenda ambazo bado hazijawekwa wazi. Lakini kikao hicho kinafanyika siku moja tu baada ya taifa hilo kumpata Rais Mpya, Samia Suluhu Hassan aliyeapishwa jana baada ya mtangulizi wake, John Magufuli kufariki dunia wiki hii,