1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABUJA. Wapelelezi wa FBI wavamia nyumba ya makamu wa rais na kufanya upekuzi

29 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEgc

Wapelelezi wa FBI nchini Marekani walivamia makaazi ya makamu wa rais wa Nigeria bwana Atiku Abubakar na kufanya upekuzi katika mji wa Maryland, Washington.

Kwa mujibu wa ripoti za magazeti upekuzi huo ulifanyika kutafuta ushahidi katika kesi ya rushwa inayomkabili mjumbe wa marekani wa jimbo la New Orleans William Jefferson wa chama cha Democrats.

Wapelelezi hao wanatafuta ushahidi iwapo mjumbe huyo alilipa au aliidhinisha malipo kwa maafisa wa Nigeria na Ghana.

Msemaji wa rais Olesegun Obasanjo bi Remi Oyo amesema, kwamba matukio hayo ni ya kibinafsi na wala hayaihusishi serikali ya Nigeria hata hivyo balozi wa Nigeria nchini Marekani amepewa maagizo ya kufuatilia maelezo zaidi juu ya tukio hilo.