Adam Masava ni miongoni mwa vijana wanaojihusisha na sanaa ya uchoraji wenye hadithi za kusisimua. Mzaliwa huyu wa Nairobi Kenya anatumia kipaji chake kujikimu kimaisha lakini pia kutoa funzo kwa jamii. Ahmad Juma alikutana naye Dar es Salaam akishiriki maonesho ya michoro yake na hapa anaangazia juhudi zake ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wasanii wengine wanaochipuka.