Wiki hii magazeti mengi yamejishughulisha na mzozo wa nchini Sudan ambako mtawala wa kijeshi ameahidi kurejesha demokrasia, Jumuiya ya ECOWAS iliamua kuindolea vikwazo Mali na Burkina Faso, kuongezeka kwa hali ya ukame katika Pembe ya Afrika na harakati za kuyaokoa maisha ya watoto wanaokabiliwa na kitisho cha njaa miongoni mwa mada nyengine. Mwandaaji ni Iddi Ssessanga