Karibu kwa mara nyingine katika udondozi wa magazeti ya hapa Ujerumani yaliyoandika kuhusu bara la Afrika wiki hii. Mtayarishaji ni Saumu Mwasimba na miongoni mada zilizogusiwa na wahariri hao ni pamoja na mgogoro wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na mazungumzo ya kwanza ya kutafuta amani katika mgogoro wa Jimbo la Tigray nchini Ethiopia.