Al Gore kupokea Tuzo ya Amani ya Nobel
10 Desemba 2007Matangazo
Aliekuwa makamu wa rais wa Marekani Al Gore na mwanasayansi mkuu wa Jopo la Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa,watapokea hii leo Tuzo ya Amani ya Nobel katika mji wa Oslo nchini Norway.Viongozi hao wamechaguliwa kwa sababu ya kuuzindua ulimwengu kuhusu hali ya dharura inayosababishwa na ongezeko la joto duniani.