1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA:Baraza la usalama wa taifa linajadili mashambulio dhidi ya vituo vya waasi wa Kikurdi

24 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7D4

Rais Abdullah Gul wa Uturuki anaongoza mkutano wa baraza la usalama wa kitaifa unaojadili uwezekano wa kuvishambulia vituo vya waasi wa Kikurdi wanaojificha kaskazini mwa Irak.

Wakati huo huo Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amefanya mazungumzo na waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown kuhusu hali ya kaskazini mwa Irak.

Baadae katika mkutano na waandishi wa habari waziri mkuu wa Uingereza amelaani mashambulio yaliyotekelezwa na kundi la waasi la PKK na kuwauwa askari 12 wa Uturuki mwishoni mwa wiki.

Bwana Erdogan amesema kuwa nchi yake haiwezi kusubiri kwa muda mrefu kungojea serikali ya Irak iwachukulie hatua waasi wa Kikurdi.

Serikali ya waziri mkuu wa Irak Nuri al Malik imetoa agizo la kuzifunga ofisi zote za chama cha wafanyakazi cha PKK nchini humo.

Bwana Al Malik amemuahidi waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uturuki Ali Babacan kwamba serikali yake itakomesha harakati za kigaidi za PKK.

Nae rais wa jimbo la Wakurdi la kaskazini mwa Irak Masud Barzani amewataka waasi wa PKK wakomeshe operesheni zao dhidi ya Uturuki.