Kwa wiki kadhaa rais wa Madagascar amekuwa akitangaza dawa ya asili ya corona, ambayo imetengenezwa na mmea wa artemisia. Siku ya Jumatano, watafiti katika Taasisi ya Max Planck walithibitisha: mmea huo una ufanisi wa kupambana na Covid-19. Sasa tafiti zaidi zinatakiwa kufanywa.