BERLIN : 1,000 waandamana kupinga ukatili dhidi ya wanawake
6 Machi 2005Matangazo
Mwezi mmoja kufuatia mauaji ya kijana wa kike wa Kituruki nchini Ujerumani watu wanaofikia 1,000 wameandamana mjini Berlin kupinga ukatili dhidi ya wanawake.
Waandamanaji waliandamana kupitia maeneo yanayokaliwa na wakaazi wengi wa Kituruki katika mji mkuu huo wa Ujerumani kutaka kukomeshwa kwa ukandamizaji wa wanawake.Hapo tarhe 7 mwezi wa Februari kijana wa kike wa Kituruki inadaiwa kuwa aliuwawa na kaka zake mjini Berlin kwa sababu familia yake ilikuwa ikipinga nyendo zake za maisha ya kujikombowa.