1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Waendesha mashtaka wana orodha ya maajenti wa CIA

22 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDAD

Mwendesha mashtaka wa Kijerumani amesema ana orodha ya maajenti wa shirika la upelelezi la Marekani CIA wanaosemekana kuwa walimteka nyara raia wa Kijerumani,Khaled El Masri na kumzuia kwa miezi mitano.Mwendesha mashtaka huyo alisema hayo wakati wa kutoa ushahidi mbele ya kamati ya wabunge mjini Berlin.Kamati hiyo inachunguza madai ya mzaliwa wa Lebanon,El Masri kuwa alitekwa nyara Macedonia mwishoni mwa mwaka 2003 kabla ya kuwasilishwa kwa CIA.Amesema kuwa maaajenti wa Kimarekani baadae walimpeleka Afghanistan na alizuiliwa mpaka alipoachiliwa huru mwezi Mei mwaka 2004,baada ya CIA kuamua kuwa yeye si yule aliekuwa akisakwa.El Masri anasema alipokuwa kizuizini,aliteswa kisaikolojia na kimwili.