1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin:Idadi ya wanawake walioambukizwa HIV yaongezeka Ujerumani.

18 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDKb

Ujerumani imesema inataka kutumia pesa zilizotengwa kupambana na virusi vya HIV na ukimwi kwa ajili ya masaibu wasichana na akina mama.

Katika mahojiano na kituo cha radio waziri wa Maendeleo wa Ujerumani Haidamarie Vitsorek- Tsoel amesema, miaka 10 iliyopita asilimia 12 ya watu walioambukizwa virusi vya HIV walikuwa ni wanawake, lakini hivi leo idadi hiyo imeongezeka maradufu na kufikia karibu asilimia 50%.

Mwezi March mwakani wizara ya Maendeleo imetayarisha mkutano wake wenyewe kuhusu Ukimwi kwa azma ya kujadili tatizo hilo.

Nae mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kwa masuala ya ukimwi barani Afrika Stephen Lewis amezilaumu nchi za magharibi kwa mwenendo wake mbaya kwa nchi za Afrika katika suala la ukimwi kwa kusema.

„Mwelekeo kuzidanganya nchi za kiafrika, bahati mbaya upo katika nchi za Magharibi. Afrika haiwezi kufanikiwa peke yake kwa sababu ni masikini mno, na sababu moja ya umasikini huo ni mwenendo huo wa nchi za magharibi“.

Hii leo itakuwa ni siku ya mwisho ya mkutano wa kimataifa wa Ukimwi unaofanyika mjini Toronto nchini Canada.