BERLIN:Sheria ya ubaguzi wa rangi,jinsia,dini yapitishwa na Bunge la Ujerumani Bundestag
17 Juni 2005Matangazo
Bunge la Ujerumani Bundestag limepitisha sheria mpya inayolenga kuzuia ubaguzi wa rangi ,jinsia,dini, na rangi.
Lakini chama cha upinzani cha Christian Demokrats kimeikosoa sheria hiyo kikisema inakwenda ndani zaidi ya mipango ya jumuiya ya Umoja wa Ulaya inayohusu suala la ubaguzi na hilo huenda likaleta mzigo mkubwa katika uchumi.
Chama hicho kimesema kitaipinga sheria hiyo kwenye baraza kuu la mikoa Bundesrat.