Biden na Netanyahu wajadili jusitishaji mapigano Gaza
13 Januari 2025Matangazo
Juhudi hizo zinafanyika zikiwa zimebaki siku chache kabla ya rais mteule wa Marekani Donald Trump hajaingia madarakani wiki ijayo.
Wapatanishi Marekani, Qatar na Misri wamekuwa kwenye mazungumzo juu ya kusitishwa mapigano tangu mwaka uliopita bila mafanikio lakini mara hii maafisa wa Marekani wamesema wanayo matumaini ya kufikiwa makubaliano.
Soma pia:Mwili wa mateka wa Israel watambuliwa
Mkuu wa shirika la ujasusi la Israel (Mossad) David Barnea na mshauri mkuu wa Rais Biden kuhusu masuala ya mashariki ya kati Brett Mc Gurk, wako mjini Doha, Qatar kwa mazungumzo.
Hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, alisema anatumai kwamba makubaliano hayo yatafikiwa kabla ya kukabidhi ofisi kwa utawala mpya chini ya Trump.