1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brahimi aondoka Urusi kuelekea China

Admin.WagnerD30 Oktoba 2012

Mjumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya nchi za Kiarabu kuhusu Syria Lakhdar Brahimi leo anatarajiwa kuanza ziara ya siku mbili nchini China baada ya kuzuru Urusi

https://p.dw.com/p/16ZHt

Brahimi anawasili China akitokea Urusi ambako alifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Urusi Sergei Lavrov kuhusu uasi unaoendelea nchini Syria. wakati huo huo mshindi wa tuzo ya amani ya Nobeli Ramos Horta ameonya juu ya Lakhdar Brahimi alikuwa mjini Moscow jana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nchi za Kigeni wa Urusi Sergei Lavrov na ataelekea China ambako anatarajiwa kufanya mazungumzo na vongozi wa serikali leo.

Urusi na China ni washirika wa Rais wa Syria Bashar al –Assad na zilipiga kura tatu za turufu kupinga maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yaliyoungwa mkono na nchi za magharibi na Kiarabu yaliyolaani utawala wa Syria kwa machafuko yanayoendelea nchini humo.

U.N.-Arab League peace envoy Lakhdar Brahimi (L) and Russia's Foreign Minister Sergei Lavrov address the media after their meeting in Moscow October 29, 2012. Brahimi expressed regret on Monday that a U.N.-brokered truce had not been more successful in Syria but said he would not let this discourage his peace efforts. REUTERS/Maxim Shemetov (RUSSIA - Tags: POLITICS)
Lakhdar Brahimi und Sergej Lavrov in MoskauPicha: Reuters

Makubaliano ya kuweka chini silaha kwa siku nne baina ya serikali na waasi wiki iliyopita yaligubikwa na ghasia huku kila upande ukiushutumu mwengine kwa kukiuka muafaka huo. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon alisema jana kuwa amesikitishwa sana kwamba pande zote zinazozozana zilishindwa kuheshimu mpango huo wa kuweka chini silaha. Ban alitoa mwito kwa jamii iliyogawanyika ya kimataifa kuungana pamoja na kusitisha umwagaji damu unaoendelea Syria.

Ndani ya Syria kwenyewe, wanaharakati wameripoti kutokea makabiliano makali na mashambulizi ya angani katika mkoa wa Kaskazini Aleppo. Wanasema waasi wamelizingira eneo ambalo kunapatikana Makao Makuu ya jeshi la anga la Syria.

Aidha wanaharakati hao pia wamesema kulikuwa na mashambulizi ya angani kwa siku ya pili mfululizo katika maeneo ya voungani mwa mji mkuu Damascus. Kwa mujibu wa Shirika la kuchunguza ukiukaji wa haki za binadaamu la Syria, watu mia moja na thelathini wameuawa katika mashambulizi hayo.

Wakati huo huo, mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Jose Ramos-Horta ameonya kuwa Syria inakumbwa na hatari ya kutumbukia katika mgogoro kama wa Somalia. Ramos-Horta ambaye alisaidia kupatikana uhuru wa Timor Mashariki anasema hali ya Syria ni hatari akiongeza kuwa waasi hawana sifa ya demokrasia na hivyo rais Bashar al-Assad ataendelea kupigania nafasi yake na ya jamii yake.

Mapigano yanaendelea kati ya waasi na vikosi vya serikali viungani mwa mji mkuu Damascus
Mapigano yanaendelea kati ya waasi na vikosi vya serikali viungani mwa mji mkuu DamascusPicha: PHILIPPE DESMAZES/AFP/Getty Images

Mshind huyo wa tuzo ya amani ameliambia shirika la habari la AFP kuwa hali nchini Syria ni vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyohusisha makundi mengi kutoka nje, serikali, na makundi yasiyo ya serikali. Anasema mzzo huo utadumu muda mrefu, kama tu Somalia, na kwa sasa haoni suluhisho lolote la haraka.

Ramos-Horta, ambaye amukuwa mstari wa mbele katika juhudi za kutafuta amani ulimwenguni, amesema Marekani na mataifa ya Ulaya yanafanya vizuri kuwa makini wakati yakishughulika na upinzani wa Syria. Lakini akaongeza kuwa ni rahisi sana kuzilaumu Urusi na China ambazo zinapinga maazimio ya Umoja wa Mataifa kumwekea shinikizo rais Assad.

Anaongeza kuwa nafasi pekee ya mabadiliko nchini Syria inaweza kutokana na jeshi, akilitaja jeshi kuwa ni chombo muhimu katika kuwaondoa madarakani viongozi waliokuwa imara kama yaliomkuta Hosni Mubarak wa Misri na aliyekuwa rais wa Indonesia Suharto .

Mwandishi: Bruce Amani: DPA/AFP

Mhariri : Mohammed Abdul-Rahman