1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAPE TOWN Mkutano kuhusu uchumi wa Afrika umeanza leo Afrika Kusini

1 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF7s

Mkutano wa kilele kuhusu uchumi wa Afrika umeanza leo mjini Cape Town Afrika Kusini. Mada kuu ya mkutano huo ni njia za kupambana na umaskini barani Afrika. Kabla mkutano huo, kiongozi mpya wa benki ya dunia, Paul Wolfowitz, alisema kwamba maendeleo ya kiuchumi ni njia mojawapo ya kupambana na umaskini barani humo.

Zaidi ya wanasiasa 650, viongozi wa mashirika na makampuni ya kibiashara na wajumbe wa mashirika ya kimataifa wanahudhuria mkutano huo wa siku tatu uliodhaminiwa na jukwaa la uchumi duniani, World Economic Forum. Wajumbe hao pia wanataka kujadili mpango wa waziri mkuu wa Uingereza bwana Tony Blair, wa kupunguza madeni na kuongeza uwekezaji barani Afrika.