1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAPE TOWN: Ndoa kati ya watu wa jinsia moja yaruhusiwa

15 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCsl

Afrika ya Kusini imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuhalalisha ndoa kati ya watu wa jinsia moja.Bunge limeamua kupitisha sheria hiyo baada ya kuungwa mkono na zaidi ya asilimia 80 ya wajumbe.Kura hiyo ilijadiliwa kwa miezi kadhaa wakati ambapo mashirika ya kidini na wahafidhina walijaribu kuizuia sheria hiyo kupitishwa bungeni.Enzi ya ubaguzi ilipomalizika nchini humo mwaka 1994,katiba mpya iliandaliwa ikipiga marufuku ubaguzi unaohusika na sababu za ukabila, jinsia na mielekeo ya kijinsia.