CAPE TOWN. Rais Thabo Mbeki awapa wanawake nafasi ya makamu wa rais
23 Juni 2005Matangazo
Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini amemteuwa bibi Phumzile Mlambo-Ngcuka kuwa makamu wake wa rais.
Bibi Phumzile aliyekuwa waziri wa madini na nguvu za nishati amechukuwa nafasi ya bwana Jacob Zuma ambaye aliyefutwa kazi wiki iliyopita baada ya kuhusishwa na madai ya kuhusika na vitendo vya rushwa.
Bwana Jacob Zuma atafikishwa mahakamani mapema wiki ijayo.
Afrika Kusini inajivunia kumpata makamu wa rais wa kike kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo.