SiasaAsia
China na Marekani zinaweza kufanya kazi pamoja zikiungana
17 Desemba 2024Matangazo
China imeyasema haya kuelekea kurejea tena madarakani rais mteule wa Marekani, Donald, Trump anaetarajiwa kuapishwa rasmi Januari 20. Wang Yi pia ameionya Marekani dhidi ya kuingilia masuala yake ya ndani na kisiwa cha Taiwan. Mataifa hayo mawili makubwa kiuchumi duniani yamekwaruzana kwa muda kufuatia masuala kadhaa kuanzia biashara na teknolojia, haki za binaadamu na China kuendelea kutaka udhibiti kamili wa kisiwa kinachojitawala chenyewe cha Taiwan. China inadai Taiwan ni sehemu ya eneo lake na imetishia kutumia nguvu kukidhibiti kimamilifu huku Marekani ikiahidi kuisaidia Taipei na njia za kujilinda.