COLOMBO: Wasichana wa shule 43 wauwawa
14 Agosti 2006Matangazo
Waasi wa kundi la Tamil Tigers nchini Sri Lanka wamesema wasichana wa shule takriban 43 wameuwawa leo na wengine 60 wakajeruhiwa katika shambulio la angani la jeshi la serikali.
Wanajeshi wa Sri Lanka wameishambulia nyumba ya watoto mayatima katika wilaya ya Mullaitivu inayomilikiwa na waasi wa Tamil Tigers.
Wakati huo huo, waasi wa kundi la Tamil Tigers wamekataa kufanya mazungumzo ya kutafuta amani na serikali, siku mbili baada ya mapigano makali kuwaua watu 186.
Msemaji wa tume inayoongozwa na Norway amesema kundi la Tamil Tigers hapo awali lilitoa matamshi ya kutaka mazungumzo ya amani yafanyike.