SiasaCroatia
Croatia yachagua rais, Milanovi apigiwa upatu kushinda
29 Desemba 2024Matangazo
Kulingana na utafiti wa maoni wa hivi karibuni, Milanovi yuko mbele ya wagombea wenzake lakini hatarajiwi kupata asilimia 50 ya kura zote. Hali ambayo inaweza kusababisha kufanyika kwa duru ya pili ya uchaguzi Januari 12.
Utafiti wa maoni unaonesha kwamba mgombea wa chama cha kihafidhina cha Croatian Democratic Union (HDZ), Dragan Primorac, pia anatarajiwa kufaulu kwa duru ya pili ya uchaguzi.
Soma pia: Mahakama ya Katiba ya Croatia yamzuwia rais kuwa waziri mkuu
Takriban wapiga kura milioni 3.8 waliosajiliwa katika nchi hiyo ambayo ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya, wanatarajiwa kushiriki.
Matokeo ya awali ya uchaguzi huo yanatarajiwa kuanza kutolewa usiku wa Jumapili.