1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DW inakuletea uchaguzi wa Ujerumani

Mohamed Dahman
9 Juni 2017

Ujerumani inaelekea katika uchaguzi hapo mwezi wa Septemba na huku dunia yote ikiiangalia. Kwa nini hususan uchaguzi huu ni mahsusi  na vipi DW itautangaza, anaelezea mhariri mkuu wa DW, Ines Pohl.

https://p.dw.com/p/2eOoJ
Deutschland Reichstag
Picha: picture-alliance/R. Goldmann

Macho yote ya dunia yako kwa Ujerumani hivi sasa kuliko ilivyowahi kuwa kabla. Wengi wanaiangalia kwa kuihusudu na kuithamini. Lakini sio wote, wengine wanashangaa, wengine wana wivu kidogo, vipi Ujerumani imeweza kudumisha utulivu kukiwa na changamoto na matatizo mengi. Wengine wanahofu kupata upya nguvu kwake ikiwa katikati ya Ulaya.

Ujerumani na Kansela wake, Angela Merkel, kwa pamoja wanaonekana kuwa matumaini ya mwisho ya Umoja wa Ulaya wakati wengine wanaona wanaweka taratibu zao sio kwa maslahi pekee ya Ulaya bali kwa faida yake likiwa kama taifa kuu lenye kusafirisha nje bidhaa kwa wingi  na taifa la miujiza ya kiuchumi.

Kwa kutegemea wapi nilipo duniani, nimekutana na watu ambao wanaona hatua ya Ujerumani ya kupokea zaidi ya wakimbizi milioni moja kama kitendo cha huruma au kwa ghadhabu wanalaumu kwa kuwa ndio mwisho wa Ukristo barani Ulaya.

Kutokana na hisia hii ya mgawanyiko kwamba sisi katika DW tunasubiri kwa hamu kampeni za uchaguzi zinazokuja. Ujerumani itapiga kura kwa ajili ya bunge jipya hapo tarehe 24 mwezi wa Septemba.

DW itakuwa nawe muda wote

Tukiwa kama kituo cha utangazaji cha kimataifa cha Ujerumani tunalenga juu ya ongezeko la zingatio kwa kile kinachotokea nchini. Kipi kinachowafanya kwa kiasi kikubwa Wajerumani watosheke na mkondo unaofuata nchi hivi sasa?

Kipi kinachosababisha wengine wahofie mustakbali na kuhisi wanawalea watoto wao katika nchi ambayo haifanani tena na ile waliyoiwazia?

Ines Pohl
Mhariri mkuu wa DW Ines PohlPicha: DW/P. Böll

Je, Ujerumani iko tayari kuwa nchi ya wahamiaji au mafanikio ya wanasiasa wa sera kali za mrengo wa kulia katika chaguzi ni ushahidi kwamba nchi inaelekea katika mwelekeo ambao hauwaridishi wapiga kura wengi?

Ziada ya hayo tutaelezea sababu za mafanikio ya kiuchumi ya Ujerumani, vipi mfumo wa elimu wa Ujerumani unafanya kazi na kipi kinaoufanya uwe tafauti. 

Tutawaleteya wasifu wa viongozi wetu wa kisiasa hususan Angela Merkel mmojawapo wa mtu mashuhuri na mwenye ushawishi mkubwa duniani ambaye anawania muhula wa nne kama kansela.

Kipi tunaweza kutaraji kutoka kwao na sera ya kigeni itafuata mwelekeo gani?

Masuali ni mengi: Muungano ina umuhimu gani hususan Jumuiya ya Kujihami ya NATO? Nani anaunga mkono maendeleo na nani anaunga mkono matumizi ya kijeshi?Ujerumani inaitathmini vipi dhima yake ndani ya Umoja wa Ulaya?

Zungumza nasi: Ujerumani ni nini?

Kwa kila kile tutakachokifanya, tunataka kiwe katika mbadilishano ya karibu na wewe, wasomaji wetu, watazamaji wetu na wasikilizaji. Kwa hashtag (#) uliza DW, waandishi wetu wataweka masuali na kusubiri kwa hamu majibu yenu. Tunataka kujuwa kujuwa vipi tunapaswa kuyaelezea masuala hayo na tunataka mawazo na fikra zenu.

Wakati tukielekea katika kampeni, tunataka kuwa jukwaa la kwa mazungumzo na dunia katika lugha 30 inazozungumza DW. Ujerumani ni nini? Dhima gani inapaswa kutimiza katika masuala ya usalama, NATO na Umoja wa Ulaya? Ni matarajio yako kwa serikali itakayochaguliwa? Unahofia nini? Ujerumani unaiona ina nguvu gani na udhaifu gani? 

Kwenye mitandao ya Twitter, Facebook, TV na katika tovuti yetu utakutana na hashtag #UjerumaniYaamua. 

Tunasubiri kwa hamu mchango wako wa maoni katika mazungumzo. Mtandao wetu wa dunia wa maripota na wafanyakazi wa uhariri mjini Berlin na Bonn wataelezea kile kinachotokea nchini Ujerumani na masuala yanayopigiwa kura ni yapi kuanzia sasa hadi siku ya uchaguzi Septemba 24.

Mwandishi: Ines Pohl/DW
Tafsiri: Mohamed Dahman
Mhariri: Yusuf Saumu