Sanaa ya graffiti yaani michoro ya maneno, inaendelea kushika kasi jijini Nairobi. Tofauti na kwingineko ambako wasanii wa Sanaa hii hawajitokezi kimasomaso. Wasanii wa graffiti wanaochipuka jijini Nairobi, wamekuwa mifano bora. Wamechukua jukumu la kuipa jamii mafunzo.