Wajomvu ni miongoni mwa makabila ya waswahili wa pwani ya Kenya. Wanajulikana kwa ustadi wao wa kutengeneza vyungu madhubuti vilivyotumiwa na watu wa pwani. Wanazungumza lahaja ambayo ni tofauti na ile ya Kiswahili cha Ki-mvita. Mengi zaidi kuhusu wajomvu, kabila lenye utajiri wa historia na utamaduni, ni kwenye makala hii ya utamaduni na sanaa ukiwa. Msimulizi ni Fathiya Omar.