1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanawake zaidi watakiwa kulindwa katika janga la corona

6 Aprili 2020

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezitaka serikali kuwajumuisha wanawake katika juhudi zao za kupambana na janga la virusi vya corona.

https://p.dw.com/p/3aVEL
Coronavirus - UN-Generalsekretär Guterres
Picha: picture-alliance/dpa/C. Zingaro

Visa vya dhuluma dhidi ya wanawake vimeongezeka kote duniani mnamo wakati serikali tofauti zimeweka marufuku ya kutotoka nje kwa ajili ya kuudhibiti kuenea kwa virusi hivyo.

Akizungumza katika ujumbe alioutoa kwa njia ya video, Guterres amezitaka serikali kuwaweka wanawake katika mipango yao ya kukabiliana na virusi hivyo.

Kulingana na tume ya kitaifa ya wanawake nchini India katika wiki ya kwanza ya marufuku ya kutotoka nje, nchi hiyo iliripoti mara mbili ya visa vya unyanyasaji wa wanawake ambavyo kawaida inaandikisha.

Na uongozi nchini Ufaransa unasema visa nchini humo viliongezeka kwa thuluthi moja huku Australia ikiripoti asilimia sabini na tano ya watu waliokuwa wanatafuta njia za kuwasaidia wahanga wa dhuluma za kinyumbani kwenye mtandao wa intaneti.