1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamas yatishia kuwaua mateka wa Israel

4 Desemba 2024

Kundi la wanamgambo la Hamas limetishia kuwaua mateka ikiwa Israel itafanya operesheni ya kuwaokoa mateka hao, kama ilivyofanya katika kambi ya Nuseirat huko Ukanda wa Gaza mnamo mwezi Juni.

https://p.dw.com/p/4nkKE
Israel I Tel Aviv - Israelis fordern die Rückkehr der im Gazastreifen entführten Geiseln
Waisraeli wakidai kurejeshwa kwa mateka waliotekwa nyara huko Gaza Tel Aviv Novemba 5, 2024,Picha: Jack Guez/AFP

Kulingana na taarifa ya ndani iliyotolewa kwa shirika la habari la Reuters, Hamas wamesema wamepata taarifa kwamba Israel inanuia kufanya operesheni kama hiyo ya kuwaokoa mateka wao. Kwenye taarifa hiyo iliyoandikwa Novemba 22, Hamas iliwaarifu wapiganaji wake kutojali madhara yoyote ya kufuata maagizo hayo na kwamba Israel ndio inahusika na hatima ya mateka hao. Waziri wa Ulinzi wa Israel Israel Katz amesema jioni hii kwamba shinikizo linaongezeka kwa Hamas na sasa watakuwa tayari kuendeleza makubaliano ya mateka hao.