Harare. Waandamanaji wanawake wakamatwa na polisi.
20 Aprili 2007Matangazo
Kiasi waandamanaji 82 wengi wao wakiwa wanawake wamekamatwa katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Zimbabwe wa Bulawayo kupinga ukosefu mkubwa wa umeme, wanaharakati wamesema leo.
Waharakati waliokamatwa , wote wakiwa waungaji mkono wa kundi la Wanawake wa Zimbabwe waamka, WOZA, walikamatwa jana alhamis baada ya kufanya mgomo wa kukaa katika ofisi za shirika la ugavi wa umeme mjini Bulawayo.
Mwanaharakati mmoja ambaye aliwapelekea chakula waandamanaji hao alikamatwa na kupigwa na polisi, amesema mratibu wa kundi hilo la WOZA Jenni Williams.