Hatua kubwa katika mazungumzo kati ya Israel na Hamas Doha
14 Januari 2025Wapatanishi wa Marekani na mataifa ya Kiarabu wamepiga hatua kubwa kuelekea kupatikana kwa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas na pia kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas katika ukanda wa Gaza.
Maafisa hata hivyo wamesema makubaliano rasmi bado hayajafikiwa.
Maafisa wanne wamekiri kwamba kumepigwa hatua na kuongeza kuwa siku zijazo zitakuwa na umuhimu mkubwa kuelekea kupatikana kwa makubaliano ya kusitisha vita vya zaidi ya miezi 15 ambavyo vimevuruga eneo la Mashariki ya Kati.
Soma pia: Kiongozi wa Hamas azungumza na wapatanishi kuhusu usitishaji vita Gaza
Maafisa hao wamezungumza kwa masharti ya kutotajwa majina kwa sababu hawajaruhusiwa kujadili kuhusu mazungumzo hayo yanayofanyika mjini Doha, Qatar.
Kiongozi Mkuu wa Qatar, Sheikh Tamin bin Hamad Al Thani, alikutana na ujumbe wa Hamas mjini Doha pamoja na Witkoff na Brett McGurk, mshauri mkuu wa Rais Joe Biden kuhusu masuala ya Mashariki ya Kati. Al Thani pia amezungumza kwa njia ya simu na Biden, ambaye amesisitiza umuhimu wa kufikia haraka iwezekanavyo makubaliano ya kusitisha mapigano.
Mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika mazungumzo ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas na kuwaachilia mateka