1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ruto: Vifo vya njaa vya makumi ya watu ni sawa na ugaidi

24 Aprili 2023

Polisi nchini Kenya imesema madhehebu ya itikadi kali ya Kikristo yamesababisha vifo vya takriban watu 60. Wahanga walilazimika kufunga hadi kufa kwa Imani kwamba wangekutana na Yesu Kristo.

https://p.dw.com/p/4QUrx
Kenia Präsident William Ruto
Picha: TONY KARUMBA/AFP

Rais wa Kenya William Ruto ameahidi kwamba msako kabambe utafanywa dhidi ya kile alichokiita kuwa matendo yasiyokubalika ya kidini.

Amesema hayo mnamo wakati polisi wakipata miili zaidi iliyozikwa kwenye kipande cha shamba ndani ya msitu wa Shakahola kaunti ya Kilifi, Pwani ya Kenya.

Polisi wamemtaja mhubiri anayeshukiwa kuwapandikisha waumini hao misimamo hiyo mikali kuwa ni Paul Mackenzie Nthenge.

Hadi kufikia sasa miili ya watu 58 imepatikana huku wengine wakiokolewa wakiwa hai, japo wakiwa hali mahututi.