1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD : Wanawake wa Kichina waachiliwa

24 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBoo

Wanafunzi wa itikadi kali za Kiislam wamewaachilia huru watu tisa wakiwemo wanawake sita wa Kichina baada ya kuwashikilia kwa takriban masaa 17.

Wanafunzi hao kutoka Msikiti Mwekundu walikivamia kituo cha tiba ya vitobo na ukandaji katika mji mkuu wa Islamabad na kuwashutumu watu hao tisa kwa kuendesha danguro.Naibu Mkuu wa msikiti huo Abdul Rashid Ghazi amesema kwamba watu hao tisa wameachiliwa kwa kuzingatia maslahi ya urafiki kati ya Pakistan na China.

Afisa mwandamizi wa serikali ya Pakistan amewaambia waandishi wa habari kwamba serikali itavifunga vituo vyote vya tiba visivyo halali katika mji mkuu huo.