1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaendeleza mashambulizi Gaza na kuuwa watu 17

28 Novemba 2024

Wapalestina 17 wameuawa kwenye mashambulizi ya kijeshi ya Israel katika Ukanda wa Gaza, wakati vikosi vya Israel vikiendeleza mashambulizi kwenye maeneo ya kati na kuvisogeza vifaru vyao kaskazini na kusini mji huo.

https://p.dw.com/p/4nWJN
Mzozo wa Mashariki ya Kati
Israel yaendeleza mashambulizi katikati ya Gaza na kuuwa watu 17Picha: Omar AL-QATTAA/AFP

Watu sita waliuauwa katika mashambulizi mawili tofauti ya angani kwenye nyumba moja na karibu na hospitali ya Kamal Adwan eneo la Beit Lahiya kaskazini mwa Ukanda wa Gaza. Watu wengine wanne waliuwawa wakati wakati shambulizi la Israel liliipiga pikipiki katika eneo la Khan Younis kusini mwa Gaza.

Katika eneo la Nuseirat, mojawapo ya kambi nane za wakimbizi huko Gaza, ndege za Israel lilifanya mashambulizi kadhaa ya angani na kuharibu jengo la ghorofa kadhaa. Watu saba waliuawa kwenye mashambulizi hayo.

Hezbollah yatangaza "ushindi" dhidi ya Israel

Madaktari wamesema watu wawili, mwanamke na mtoto, waliuawa katika shambulizi lililofanywa na kifaru kwenye maeneo ya magharibi ya Nuseirat, wakati shambulizi ya angani liliuwa watu wengine watano katika nyumba iliyokuwa karibu.

Makubaliano yanaendelea kuzingatiwa juu ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hezbollah, mshirika wa Hamas nchini Lebanon, tangu yalipoanza kutekelezwa jana.