1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yalaumiwa kwa kuzuia usambazaji maji Gaza

19 Desemba 2024

Shirika la Human Rights Watch, limeilaumu Israel kwa kusababisha vifo vya maelfu ya Wapalestina kwa kuzuia na kulenga usambazaji wa maji katika Ukanda Gaza, hatua ambazo limezitaja kuwa za mauaji ya kimbari.

https://p.dw.com/p/4oNC3
Mashambulizi ya Israel Gaza
Israel inasisitiza kwamba Hamas ndio inayohusika na uharibifu huo kwa kutumia shule, hospitali, na maeneo ya makazi Picha: Hani Alshaer/Anadolu/picture alliance

Ripoti ya Human Rights Watch imesema vichanga, watoto na watu wazima wamekufa kutokana na utapiamlo, upungufu wa maji mwilini, na magonjwa, kufuatia hatua za Israel za kukata maji, umeme, kuharibu miundombinu, na kuzuia usambazaji wa misaada muhimu.

Soma pia: Israel inataka kuwa na udhibiti kamili wa usalama mjini Gaza baada ya usitishwaji mapigano

Israel imekanusha madai haya, ikisema vita vyake vinalenga wapiganaji wa Hamas na si raia wa Gaza. Huma Rights Watch iliongeza kuwa muundo wa vitendo vya Israel na matamko ya maafisa wake vinaweza kuashiria nia ya mauaji ya kimbari, ingawa uthibitisho wa nia hiyo ni muhimu chini ya sheria za kimataifa.

Israel inasisitiza kwamba Hamas ndio inayohusika na uharibifu huo kwa kutumia shule, hospitali, na maeneo ya makazi kwa operesheni zake.