Rais Samia Suluhu Hassan ameendelea kuonesha kuwa kiongozi anayewaamini wanawake katika nyadhifa mbali mbali za uongozi nchini Tanzania. Hii ni tafsiri iliyojitokeza na kuibua mijadala baada ya rais huyo kupitisha jina la naibu Spika wa bunge la Tanzania, Tulia Ackson, kuwa mgombea wa nafasi ya spika. Je ni mwelekeo mpya? Saumu Mwasimba amejadili na mchambuzi wa kisiasa Profesa Benson Bana.