1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Jeshi la Israel lateketeza hospitali ya Gaza kwa moto

28 Desemba 2024

Shirika la Afya Duniani limesema operesheni ya kijeshi ya Israeli karibu na Hospitali ya Kamal Adwan imeifanya hospitali hiyo, ambayo ni kituo cha mwisho kikubwa cha afya kaskazini mwa Gaza, kusitisha huduma zake.

https://p.dw.com/p/4odcE
Ukanda wa Gaza Bait Lahia | Uharibifu Hospitali ya Kamal Adwan
Watumishi wa afya wakiwaondoa wagonjwa wa saratani na majeruhi kutoka hospitali ya Kamal Adwan iliyoko Beit Lahia, kaskazini mwa Gaza, Oktoba 28, 2024.Picha: AFP/Getty Images

Wanajeshi wa Israeli walivamia na kuchoma moto Hospitali ya Kamal Adwan kaskazini mwa Gaza, baada ya kuwaondoa kwa nguvu wagonjwa na wafanyakazi, Wizara ya Afya ya Gaza imesema, huku jeshi la Israeli likidai hospitali hiyo ilitumika na wapiganaji wa Hamas kama kituo, bila kutoa ushahidi.

Soma pia: Shambulizi la Israel lauwa waandishi watano wa Kipalestina

Jeshi la Israeli lilikanusha kuwajibika moja kwa moja kwa moto mkubwa uliotekeza hospitali hiyo, likisema ni jengo tupu lililoathirika.

Wakati huo huo, mwanamke wa miaka 83 aliuawa kwa kuchomwa kisu na Mpalestina kutoka Ukingo wa Magharibi nchini Israeli, huku jeshi la Israeli likisema limezuia kombora lililorushwa na waasi wa Kihuthi kutoka Yemen, ambao walisema mashambulizi yao hayatakoma mpaka Israel ikubali usitishaji wa mapigano Gaza.