1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Jeshi la Kongo lamkamata mwanajeshi wa Rwanda

27 Desemba 2024

Jeshi la kongo FARDC limetangaza kuwakamata askari wa kikosi maalum kutoka jeshi la Rwanda wakati wa mapigano huko wilayani Lubero mkoani kivu kaskazini.

https://p.dw.com/p/4ocPK
Askari wa FARDC
Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo - FARDC wanapambana na makundi ya waasi mashariki ya nchi hiyoPicha: Djaffar Sabiti/REUTERS

Mbele ya vyombo vya habari, askari huyo aliyekamatwa alithibitisha uwepo wao kwenye ardhi ya kongo kuwasaidia waasi wa M23 wanaopigana dhidi ya jeshi la kongo. HAKIZIMANA IRADUKUNDA ni miongoni mwa wanajeshi wengine wa Rwanda waliokamatwa  jumamosi iliyopita kati ya vijiji vya Mambasa na Ndoluma wakati wa mapigano baina ya jeshi la Kongo na waasi wa M23 wilayani Lubero.

Soma pia: Rais wa Kongo afanya mabadiliko makubwa jeshini

Akioneshwa mbele ya vyombo vya habari hiyo jana alahamisi , askari huyo kutoka kitengo maalumu cha jeshi la Rwanda alithibitisha kuwepo kwao kwenye ardhi ya kongo.

Tshisekedi: Amani imo mikononi mwa rais atakayemrithi Kagame

Serikali ya Kinshasa hata hivyo ,inaishutumu Kigali kwa kuwapeleka zaidi ya wanajeshi 4,000 katika eneo lake, hasa upande wa jimbo la kivu kaskazi, ambako mapigano yameongezeka katika miezi ya hivi karibuni.

Shutuma hizi zinaungwa mkono na ripoti  za umoja wa mataifa,ambazo zinathibitisha kwamba vikosi vya Rwanda vinalisaidia kundi la waasi wa M23 ,lakini pia vinatekeleza uingiliaji wa kijeshi wa moja kwa moja. akiuhutubia mkutano wa vyombo vya habari, Lt kanali MAK HAZUKAY msemaji wa jeshi la kongo katika mapigano hayo yanayo shika kasi huko wilayani Lubero, amesema kwamba wilaya ya Lubero imekuwa ni kitovu cha mapigano kati ya waasi hao wanaoungwa mkono na Rwanda na vikosi vya usalama vya kongo baada ya kuvunjika kwa mazungumzo kati ya DRC na Rwanda. 

Vita hivyo vinavyochukua sura mpya ,vimewafanya maelfu wa raia kukimbia nyumba zao baadhi wakielekea mjini Butembo na wengine kukwama msituni hali inayoongeza wasiwasi katika eneo hilo lenye watu wengi.