KABUL.Mkuu wa kitengo cha maswala ya wanawake auwawa
25 Septemba 2006Matangazo
Watu wasiojulikana wamemuuwa afisa wa cheo cha juu aliyekuwa akishughulikia maswala ya wanawake katika eneo la kusini mwa mkoa wa Kandahar nchini Afghanistan.
Bibi Safia Hama Jan aliuwawa kwa kupigwa risasi na wanaume wawili waliokuwa juu ya pikipiki wakati alipokuwa akitoka nyumbani kwake kuelekea kazini.
Bibi Jan alikuwa mkuu wa kitengo cha maswala ya wanawake alichokiongoza tangu mwaka 2001 muda mfupi baada ya kupinduliwa kwa utawala wa Taliban.