1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kada wa upinzani apatikana na majeraha baada ya 'kutekwa'

2 Desemba 2024

Mwanachama wa upinzani ACT Wazalendo, aliyedaiwa kutekwa amepatikana usiku katika fukwe za jiji la Dar Es Salaam akiwa na majeraha.

https://p.dw.com/p/4ndNx
Kumekuwa na madai ya visa vingi vya utekaji Tanzania katika miezi ya hivi karibuni
Kumekuwa na madai ya visa vingi vya utekaji Tanzania katika miezi ya hivi karibuniPicha: Ericky Boniphase/DW

Chama cha upinzani nchini Tanzania ACT Wazalendo kimeeleza kuwa mkuu wa tawi la vijana wa chama hicho Abdul Nondo ambaye wanadai alitekwa jana na vikosi vya usalama, alipatikana usiku katika fukwe za jiji la Dar Es Salaam akiwa na majeraha na sasa amelazwa hospitalini.

Chama hicho kilisema Nondo alikamatwa katika kituo cha mabasi alipokuwa akirejea kutoka mkoani Kigoma mashariki mwa Tanzania. Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Bara Isihaka Mchinjita ameandika kwenye ukurasa wa X  kuwa ukatili wanaopitia vijana, utaligeuza taifa hilo kuwa uwanja wa fujo na visasi.

Hayo yanajiri siku chache baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi za serikali za mitaa ambao baadhi ya vyama vya upinzani vinataka ufutwe kutokana na kasoro nyingi zilizoshuhudiwa.