1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Angela Merkel akosoa jela za siri za CIA

9 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDDz

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ameikosoa Marekani kwa kuendeleza jela za siri za idara ya upelelezi ya CIA.Jela kama hizo anasema kansela Angela Merkel haziambatani na taratibu na nchi zinazoheshimu sheria .Lawama zimetolewa pia na waziri wa mambo ya ndani Wolfgang Schäuble aliyesema tunanukuu:”hata marafiki zetu wa Marekani wanabidi pia waheshimu misingi ya sheria.”Mwisho wa kumnukuu waziri wa mambo ya ndani wa serikali kuu ya Ujerumani Wolfgang Schäuble.Rais George W. Bush amekiri jumatano iliyopita kwamba idara ya upelelezi ya CIA ilikua ikishikilia jela kadhaa za siri katika kila pembe ya dunia ambako watuhumiwa wa kigaidi walikua wakishikiliwa.