Kenya yatangaza mpango wa kuanza kuwafidia wafugaji
24 Julai 2023Matangazo
Kulingana na katibu katika wizara ya maeneo kame Idris Dokata, hatua hiyo inapania kuwapiga jeki wafugaji walioathirika pakubwa na kiangazi cha muda mrefumwaka jana.
Katibu huyo ameeleza kwamba, serikali imeweka mbinu mwafaka ya kuzitambua familia zilizoathirika zaidi kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.
Soma pia:Serikali yawatafutia maji wafugaji Kenya
Wakati huohuo, serikali imefafanua kwamba,imeongeza msaada wa chakula kwa wakaazi katika maeneo yaliyoripoti ukame mwaka jana.
Katika jimbo la Marsabit, serikali inalenga kuzifidia angalau familia 1200 zilizoathirika na ukame.