Kigali:Mkutano wa wanawake barani Afrika
22 Februari 2007Matangazo
Mkutano wa wanawake barani Afrika unaanza leo katika mji mkuu wa Rwanda-Kigali.Rwanda ni nchi inayoongoza duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya wabunge wanawake duniani wakiwa karibu nusu ya wabunge wa nchi hiyo.
Mkutano huo utafunguliwa na Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf ambaye amealikwa kuwa mgeni Rasmi. Rais Sirleaf ni Rais wa kwanza mwanamke barani Afrika, na kuchaguliwa kwake kuiongoza Liberia, kumegeuka mfano katika juhudi za kupigania usawa wa jinsi na ukombozi mwa wanawake barani humo.