Kimbunga Chido chauwa watu 13 Malawi
19 Desemba 2024Huku kimbunga hicho kikiwa kimepoteza nguvu baada ya kusafiri zaidi ya kilomita 500 barani, kiliwajeruhi takriban watu 30 na kuathiri zaidi ya watu 45,000 wakati kilipopita Malawi Jumatatu.
Soma pia: Rais Macron awasili Mayotte kutathmini uharibifu wa kimbunga
Idara hiyo imesema kati ya kaya 10,159 zilizoathirika, watu 227 wamepoteza makazi. Ripoti ya idara hiyo imekuja wakati ambapo Malawi, moja ya nchi maskini zaidi duniani, inakabiliwa na changamoto kubwa za kiuchumi, huku asilimia 71 ya wananchi wake wakiishi katika umasikini wa kupindukia.
Kulingana na mamlaka ya Mayotte, Kimbunga Chido kimeua watu 31 na kujeruhi zaidi ya 1,000 katika eneo hilo la Bahari ya Hindi. Kwa upande wa Msumbiji, ripoti rasmi iliyotolewa Jumatano ilisema kuwa kimbunga hicho kimesababisha vifo vya watu wasiopungua 45 na kujeruhi takriban 500 wengine.