Maisha katika wilaya za Rufiji na Kibiti, mkoa wa Pwani nchini Tanzania yanatajwa kuwa yamekwama kutokana na kuendelea kwa mauaji ya kikatili ya viongozi wa serikali za mitaa na chama tawala CCM kwa baadhi ya maeneo ya mkoa wa Pwani huku kukiwa na masuala mengi. Wahusika ni nani, kwa nini wanafanya hayo? Mohamed Dahman anajadili suala hilo na waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania Mwigulu Nchemba.