1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Korea Kusini yawapiga marufuku ya kusafiri maafisa zaidi

10 Desemba 2024

Maafisa nchini Korea Kusini wamewapiga marufuku maafisa wengine wakuu kuondoka nchini humo.

https://p.dw.com/p/4nyOn
Rais Yoon Suk Yeol wa Korea Kusini
Rais Yoon Suk Yeol wa Korea Kusini.Picha: South Korean Presidential Office/Yonhap/AP/picture alliance

Inafuatia jaribio lililoshindwa la Rais Yoon Suk Yeol kutangaza sheria ya kijeshi. Siku moja baada ya Yoon mwenyewe kupigwa marufuku ya kusafiri, chama chake kinaendelea na mkakati wa kujiuzulu ambao inasemekana utamfanya aachie madaraka Februari mwakani au Machi kabla ya kuitishwa uchaguzi mpya. Nao wapinzani wanapanga kuwasilisha kila Jumamosi kura ya kumvua madaraka.

Maafisa wanamchunguza rais huyo na washirika wake kwa tuhuma za uasi kutokana na mfululizo wa matukio yaliyoshuhudiwa nchini humo alipotangaza sheria ya kijeshi ambayo kisha aliibatilisha kutokana na shinikizo la bunge.

Kamishna mkuu wa polisi ya Korea Kusini Cho Ji-ho, na maafisa wengine wawili waandamizi wa polisi wamezuiwa kusafiri nje ya nchi. Tayari mawaziri wa zamani wa ulinzi na mambo ya ndani na kamanda wa sheria ya kijeshi Jenerali Park An-su wamewekwa chini ya vikwazo vya kusafiri na walihojiwa leo bungeni.