1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KUWAIT: Sheria ya kuwawezesha wanawake kupiga kura yagonga mwamba

3 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFHK

Juhudi za kuwawezesha kupiga kura na kusimama katika uchaguzi wa mabaraza ya miji wanawake wa Kuwait kwa mara ya kwanza zimegonga mwamba baada ya bunge kushindwa kupitisha sheria hiyo hapo jana.

Ijapokuwa wabunge 29 walipigia kura ya kuunga mkono sheria hiyo idadi sawa na hiyo haikupiga kura huku kura mbili zikipinga sheria hiyo.Hii inafuatia baada ya kupitishwa kwa sheria hiyo wiki iliyopita katika raundi ya kwanza ya kuipigia kura.

Hata hivyo bado haijabainika iwapo sheria itapigiwa tena kura.

Sheria iliyoko hivi sasa ya kupiga kura inakataza wanawake nchini Kuwait kupiga kura au kusimama katika uchaguzi licha ya katiba ya nchi hiyo kusisitiza juu ya usawa wa kijinsia.