KUWAIT Wanawake wachaguliwa kuwa viongozi nchini Kuwait
6 Juni 2005Matangazo
Serikali ya Kuwait imewataja wanawake wawili kuwa viongozi wa baraza la mji, kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo. Bunge la nchi hiyo lilipiga kura mwezi uliopita kuwapa wanawake haki kamili za kupiga kura nchini humo. Wanawake wataruhusiwa kupiga kura kwa mara yao ya kwanza katika uchaguzi wa mwaka wa 2007.