KUWAIT: Wanawake wapewa haki ya kupiga kura
17 Mei 2005Matangazo
Bunge nchini Kuwait limepitisha sheria inayowapa wanawake haki ya kupiga kura na kugombea uchaguzi kwa mara ya mwanzo.Spika wa bunge Jassim al-Khorafi amesema,sheria hiyo imepitishwa kwa uwingi mkubwa katika bunge lenye wanaume watupu.Lakini wanaharakati wa kike wanasema sheria hiyo haijapitishwa mapema vya kutosha,kuwaruhusu wanawake kupiga kura na kogombea chaguzi za mitaani zilizopangwa kufanywa tarehe 2 mwezi Juni.