1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Leo ni Siku ya Wanawake Duniani

8 Machi 2006

Leo ni siku ya wanawake duniani, siku hii imeadhimishwa kwa kampeni mbali mbali huku utoaji mimba, dhulma za kimapenzi na biashara ya kuuza watu wengi wao wakiwa wanawake zikiwa ndizo mada zilizo mulikwa zaidi katika kuisherehekea siku hii.

https://p.dw.com/p/CHnh
Wanawake wa Somalia wapinga ukeketaji
Wanawake wa Somalia wapinga ukeketajiPicha: dpa

Siku hii imeadhimishwa kwa maandamano makubwa huko mjini Hong Kong ambako waandamanaji wameapa kupambana na visa dhulma za kimapenzi na kutengwa kwa wanawake katika bara Asia.

Nchini Marekani nako wanaharakati wa kutetea haki za wanawake wamefanya mjadala na kuliangalia kwa undani swala la haki ya utoaji mimba, siku mbili baada ya gavana wa jimbo la Dakota Kusini kutaka ibatilishwe sheria hiyo iliyopitishwa mwaka 1973 ambayo ilihalalisha utoaji mimba nchini humo.

Hakuna mtu anaejua kwa uhakika idadi ya wanawake wanaotumikishwa kama makahaba duniani ama idadi ya wale wanaofanyishwa kazi za vibarua kwa ujira wa chini sana.

Mkuu wa kitengo cha kimataifa cha kupambana na biashara ya kuuza watu bwana Richard Danzinger amezilaumu idara za polisi na uhamiaji kwa kushirili katika kuwanyanyasa wanawake.

Otton.

Ubaguzi dhidi ya wanawake hao unafanywa na idara za polisi na uhamiaji katika nchi ambapo wanawake hao wanapelekwa iwe katika nchi za ulaya magharibi ama kwengineko.

Kuhusu ubaguzi unaofanywa dhidi ya akina mama duniani, rais wa tume ya bara la ulaya bwana Jose barroso amelalamika kwamba akina mama hao wanalipwa mishahara pungufu yaile wamayolipwa wanaume kwa kazi zile zile wanazofanya.

Otto.

Pia katika medani ya siasa wanawake wanapunjika kwa sababu hawa wakilishwi katika kiwango kinachostahili, hali hiyo inawakabili wanwake barani ulaya, Afrika na katika sehemu zingine.

Huko nchini Afghanistan wakati ambapo wanawake wamo katika hatua za kujikwamua na ubaguzi baada ya nchi hiyo kukumbwa na vita vya miaka mitano chini ya utawala wa Taliban, Katika siku hii ya wanawake duniani wanawake nchini Afghanistan wameanzisha mpango wa kutathmini visa vya ubakaji nchini humo.

Nchini Pakistan siku hii kwa mara ya kwanza wanaume na wanawake wa nchi hiyo watakutana katika mkutano mkubwa ulioandaliwa na kuiadhimisha siku hii, itakumbukwa kwamba Pakistan iligonga vyombo vya habari vya kimataifa kuwa ni nchi iliyo kithiri kwa vitendo vya kuwanyanyasa wanawake hasa pale kesi ya bibi Mukhtaran Mai iliposikika duniani kote wakati alipojaribu kuwafikisha mahakamani watu waliombaka na pia kupinga adhabu aliyoipata yeye kwa niaba ya uhusiano wa kimapenzi wa kaka yake na mwanamke mwingine.

Huko Australia na New Zealand ambako wanawake wanashikilia angalau robo ya viti vya bunge hakuna shamra shamra nyingi zilizoripotiwa ingawaje watetezi wa haki za wanawake wameonya kuwa harakati za kutetea haki ya kijinsia bado zitaendelea.

Hakuna sherehe zozote kubwa zilizo andaliwa nchini Japan siku moja baada ya zaidi ya watu 10,0000 kuandamana mjini Tokyo kupinga azimio la kutaka kuwaruhusu wanawake kutawala nchi hiyo yenye falme ya kale zaidi ulimwenguni.

Huku maandamano na mijadala ya kutetea haki za wanawake ikiendelea katika nchi mbali mbal, siku hii inaelekea kupita bila kujulikana katika nchi ambazo tayari wanawake wameshapata ufanisi mkubwa wa kisiasa na uchumi.

Kutoka idhaa ya kiswahili ya radio DW tunawatakiwa wanawake duniani, siku njema na mafanikio.