LONDON: Hakuna maendeleo makubwa kupunguza mwanya wa jinsia
17 Mei 2005Matangazo
Ujerumani ni miongoni mwa nchi kumi za mbele zinazopunguza mwanya wa jinsia kati ya wanawake na wanaume.Hayo ni kwa mujibu wa uchunguzi mpya wa kimataifa.Lakini nchi za Skandinavia zinapiga fora kupunguza tofauti za jinsia,huku Sweden ikiongoza na ikifuatwa na Norway na Iceland.Uchunguzi wa nchi 58 uliofanywa na WEF huonyesha kuwa hakuna nchi yo yote ile iliyofanikiwa kuliziba kabisa pengo la jinsia.Miongoni mwa nchi zilizofanyiwa uchunguzi,India,Pakistan,Uturuki na Misri zimetenda vibaya kabisa kupunguza mwanya kati ya wanawake na wanaume.Ripoti ya WEF vile vile imeikosoa vikali Marekani,iliyochukua nafasi ya 17 na ikipitwa na nchi nyingi za Ulaya ya Magharibi.