LONDON: Mafuriko ya Tsunami yamechukua maisha ya wanawake wengi
26 Machi 2005Matangazo
Idadi ya wanawake waliopoteza maisha yao katika mafuriko ya Tsunami miezi mitatu iliopita katika nchi za Asia,ni mara nne zaidi ya ile idadi ya wanaume waliouawa katika baadhi ya nchi hizo. Shirika la misaada ya kimataifa-Oxfam,katika ripoti yake limesema wanawake waliathirika zaidi kwa sababu wakati huo,wanawake hao walikuwepo pwani wakiwangojea waume zao waliokwenda kuvua samaki au walikuwepo nyumbani pamoja na watoto.Takwimu hizo zimepatikana baada ya uchunguzi kufanywa katika maeneo yalioathirika nchini Indonesia,India na Sri Lanka.Kwa mujibu wa Oxfam,idadi kubwa ya wanaume waliobakia kulinganishwa na ile ya wanawake wachache,katika miaka ijayo huenda ikasababisha matatizo.