LONDON : Uchunguzi wa kubakwa kwa wanawake wa Kenya
14 Desemba 2006Matangazo
Uchunguzi wa kijeshi wa Uingereza umeshindwa kupata ushahidi wa kutosha kuunga mkono madai ya wanajeshi wa Uingereza kuwa wamewabaka mamia ya wanawake wa Kenya wakati wanajeshi hao wakiwa kwenye shughuli za mazoezi nchini Kenya kuanzia miongo mingi iliopita.
Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imechapisha matokeo ya uchunguzi huo wa polisi wa kijeshi baada ya timu ya takriban maafisa 20 kuchunguza zaidi ya madai 2,000 ya ubakaji katika kipindi cha miaka 55.
Gazeti la Times limesema wachunguzi waliwahoji walalamikaji wote 2,187 wengi wao wakiwa ni wanawake wa makabila ya Wamasai na Wasamburu ambao walidai fidia ya paundi milioni 20 kutoka kwa jeshi la Uingereza kutokana na madai hayo ya ubakaji.