1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maafisa wa CIA wauawa

1 Januari 2010

Maafisa 8 wa CIA wameuawa nchini Afghanistan, katika shambulizi baya kabisa dhidi ya CIA.

https://p.dw.com/p/LIDk
Maafisa 8 wa CIA wauawa, Afghanistan.Picha: DPA

Shirika la Upelelezi la Marekani, CIA, limeapa kulipiza kisasi mauaji ya maafisa wake wanane waliouawa baada ya kutokea mripuaji wa kujitoa mhanga nchini Afghanistan. Shirika hilo la Upelelezi pia limeanzisha uchunguzi kubainisha iwapo hakukuwepo na usalama wa kutosha uliomuezesha mripuaji huyo kuingia na miripuko katika eneo maafisa hao wa CIA walikuwa wanafanyia mkutano wao. Kundi la Tliban limedaia mripuaji huyo alikuwa afisa wa kijeshi wa Afghanistan ambaye analiunga mkono kundi hilo la Taliban. Rais Barack Obama aliomboleza vifo vya maafisa hao wa upelelezi. Shambulizi hilo ndilo baya kabisa dhidi ya maafisa wa CIA tangu lile shambulio la mwaka wa 1983 katika ubalozi wa Marekani mjini Beirut. Maafisa wanane waliuawa katika uripuaji huo wa bomu.